Wikimedia Foundation Chief Executive Officer/Updates/April 2024 Update/sw: Difference between revisions

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Line 13: Line 13:
* '''Malengo thabiti, kazi ya kurudia-rudia:''' Malengo manne makuu ya mpango wa mwaka huu pia yanasalia kuwa sawa na ya mwaka jana (Miundombinu, Usawa, Usalama na Uadilifu, na Ufanisi), huku kazi na yanayoweza kufikiwa ndani ya kila lengo yakirudia maendeleo yaliyopatikana katika mwaka huu. Kwa pamoja, malengo hayo manne ni mwongozo wa kuboresha teknolojia inayowezesha miradi ya Wikimedia, kusaidia na kuwezesha jumuiya zetu za kimataifa, kulinda maadili yetu, na kufanya hivyo kwa ubora na kwa ufanisi kwa mwaka huu ujao.
* '''Malengo thabiti, kazi ya kurudia-rudia:''' Malengo manne makuu ya mpango wa mwaka huu pia yanasalia kuwa sawa na ya mwaka jana (Miundombinu, Usawa, Usalama na Uadilifu, na Ufanisi), huku kazi na yanayoweza kufikiwa ndani ya kila lengo yakirudia maendeleo yaliyopatikana katika mwaka huu. Kwa pamoja, malengo hayo manne ni mwongozo wa kuboresha teknolojia inayowezesha miradi ya Wikimedia, kusaidia na kuwezesha jumuiya zetu za kimataifa, kulinda maadili yetu, na kufanya hivyo kwa ubora na kwa ufanisi kwa mwaka huu ujao.
* '''Fedha na bajeti:''' Mpango pia unajumuisha maelezo kuhusu muundo wa kifedha wa Shirika na bajeti yetu. Bajeti ya Shirika inaonyesha mabadiliko yanayoendelea, tunapoona kasi ya ukuaji wa mapato inapungua. Ili kukidhi ukweli huu mpya, Shirika limepunguza ukuaji wake kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kupunguza utumishi na gharama mwaka jana. Tangu 2022, ufadhili kwa mashirika mengine ya harakati umepita kasi ya ukuaji wa Shirika, kitu ambacho kinasalia kuwa muhimu katika mpango wa mwaka huu.
* '''Fedha na bajeti:''' Mpango pia unajumuisha maelezo kuhusu muundo wa kifedha wa Shirika na bajeti yetu. Bajeti ya Shirika inaonyesha mabadiliko yanayoendelea, tunapoona kasi ya ukuaji wa mapato inapungua. Ili kukidhi ukweli huu mpya, Shirika limepunguza ukuaji wake kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kupunguza utumishi na gharama mwaka jana. Tangu 2022, ufadhili kwa mashirika mengine ya harakati umepita kasi ya ukuaji wa Shirika, kitu ambacho kinasalia kuwa muhimu katika mpango wa mwaka huu.
Hatimaye, rasimu ya mpango huu inafika wakati wa mazungumzo ya jumuiya kuhusu Mkataba wa Harakati unaopendekezwa, ambao utapigiwa kura na Wanajumuiya hapo mwezi Juni 2024. Kwa kuzingatia kanuni za [[Special:MyLanguage/Movement Strategy/Principles#Subsidiarity & Self-Management|ukaimishaji]] na [[Special:MyLanguage/Movement Strategy/Principles#Efficiency|ufanisi]], Shirika la Wikimedia Foundation linasalia kujitolea kushirikisha na kuhamisha majukumu ambayo mashirika mengine ya Wikimedia yana vifaa vya kutosha kuweza kumiliki.
Mwisho, rasimu ya mpango huu inafika wakati wa mazungumzo ya jumuiya kuhusu Mkataba wa Harakati unaopendekezwa, ambao utapigiwa kura na Wanajumuiya hapo mwezi Juni 2024. Kwa kuzingatia kanuni za [[Special:MyLanguage/Movement Strategy/Principles#Subsidiarity & Self-Management|ukaimishaji]] na [[Special:MyLanguage/Movement Strategy/Principles#Efficiency|ufanisi]], Shirika la Wikimedia Foundation linasalia kujitolea kushirikisha na kuhamisha majukumu ambayo mashirika mengine ya Wikimedia yana vifaa vya kutosha kuweza kumiliki.


Shirika limenufaika kutokana na ushirikiano wa mara kwa mara na wa moja kwa moja na Kamati ya Uandishi wa Mkataba wa Harakati (MCDC), na mazungumzo na washikadau wengi duniani kote ili kufahamisha na kuunda [[Special:PermaLink/26310743#Wikimedia Foundation perspectives on the Global Council|mitazamo yake kuhusu majukumu ya baadaye]]. Bodi ya Wadhamini na uongozi pia walijadili hali tofauti, ikiwa ni pamoja na MCDC, kutathmini utayari wa Shirika kufanya mabadiliko ya hali ilivyo kuanzia sasa - na bila kutegemea matokeo ya uidhinishaji. Tayari tunatayarisha majukumu haya ili yasimamiwe kwa pamoja na watu wanaojitolea kwani mabadiliko endelevu huchukua muda, na ili kuyafanya vyema, mabadiliko ya kimuundo yatahitaji kuanza kwa mashauriano ya makini kuanzia sasa:
Shirika limenufaika kutokana na ushirikiano wa mara kwa mara na wa moja kwa moja na Kamati ya Uandishi wa Mkataba wa Harakati (MCDC), na mazungumzo na washikadau wengi duniani kote ili kufahamisha na kuunda [[Special:PermaLink/26310743#Wikimedia Foundation perspectives on the Global Council|mitazamo yake kuhusu majukumu ya baadaye]]. Bodi ya Wadhamini na uongozi pia walijadili hali tofauti, ikiwa ni pamoja na MCDC, kutathmini utayari wa Shirika kufanya mabadiliko ya hali ilivyo kuanzia sasa - na bila kutegemea matokeo ya uidhinishaji. Tayari tunatayarisha majukumu haya ili yasimamiwe kwa pamoja na watu wanaojitolea kwani mabadiliko endelevu huchukua muda, na ili kuyafanya vyema, mabadiliko ya kimuundo yatahitaji kuanza kwa mashauriano ya makini kuanzia sasa:

Revision as of 06:26, 20 April 2024

Salaam kwa wote,

Katika barua pepe yangu ya hivi karibuni mwishoni mwa Februari, niliwashirikisheni mada kutoka kwenye mpango unaoitwa Mazungumzo: 2024 ambapo uongozi wa Shirika, wafanyakazi, na Wadhamini walizungumza na wengi wenu katika mazungumzo yaliyokusudiwa kutayarisha mchakato wetu wa kupanga. Mapema leo, Shirika la Wikimedia Foundation lilichapisha rasimu ya Mpango wa Mwaka kwa mwaka ujao wa fedha wa 2024-2025.

Mpango wa Mwaka huu wa Mwaka wa fedha unakuja wakati wa kutokuwa na uhakika, tete na utata kwa ulimwengu mzima na kwa harakati za Wikimedia. Ulimwenguni, jukumu la habari zinazoaminika mtandaoni linazidi kuwa muhimu na kutishiwa zaidi kuliko hapo awali. Mashirika na majukwaa ya mtandaoni lazima yajielekeze kuendana na mtandao unaobadilika ambao umegawanyika zaidi na kumegukameguka. Njia mpya za kutafuta taarifa, ikiwa ni pamoja na utafutaji unaotegemea gumzo, zinazidi kuvutia. Urahisi wa kuunda maudhui yanayotokana na mashine ya Akili Bandia(AI) hutengeneza fursa na hatari kwa jukumu la Wikimedia kama mfumo wa maarifa unaoongozwa na binadamu, unaowezeshwa na teknolojia, pamoja na muundo wa kifedha wa Wikimedia.

Maoni machache kuhusu rasimu ya Mpango wa Mwaka wa mwaka huu:

  • Mkakati wa kufikia 2030: Tunapokabiliana na changamoto hizi, upangaji wa kila mwaka na wa miaka mingi wa Shirika unaendelea kuongozwa na Mwelekeo wa Kimkakati wa 2030. Mabadiliko katika ulimwengu unaotuzunguka hufanya mwelekeo huu kuwa muhimu zaidi kuliko hapo awali. Wito wa kuwa miundombinu muhimu ya mfumo ikolojia wa maarifa bila malipo ni zaidi ya kauli ya kutia moyo - ni jukumu la kuendelea kutathmini uendelevu wa miradi na mashirika yetu katika kukabiliana na mabadiliko ya mazingira yanayotuzunguka.
  • Mpango wa Miaka mingi hadi mipango ya vizazi vingi: Na lazima tujipange zaidi. Kuangalia zaidi ya 2030 ni muhimu kwa dhamira yetu, ambayo inahitaji Shirika kusaidia "kutengeneza na kuweka taarifa muhimu ... zipatikane kwenye mtandao bila malipo, katika hali ya kudumu." Mabadiliko kutoka kwa usanifu wa utafutaji wa kwa njia ya kiungo - ambao umesaidia miradi na muundo wetu wa kifedha hadi kufikia hatua hii - hadi usanifu wa utafutaji kwa njia ya kuchati uko katika siku zake za mwanzo lakini kuna uwezekano ukabaki hapa. Tunaamini kuwa hii ni sehemu ya mabadiliko makubwa katika jinsi watu wanavyounda na kutumia taarifa mtandaoni. Kinachojitokeza ni kitendawili cha kimkakati: Miradi ya Wikimedia inazidi kuwa muhimu zaidi kwa miundombinu ya maarifa ya mtandao huku wakati huo huo inapungua kuonekana kwa watumiaji wa mtandao. Ili kuhakikisha mafanikio ya miradi ya Wikimedia katika siku zijazo, ni lazima tuzingatie mbinu ya vizazi vingi katika maeneo muhimu ya upangaji wa siku zijazo.
  • Mitindo: Kama tulivyofanya mwaka jana, Shirika lilianza kupanga kwa kuuliza, "Ulimwengu unahitaji nini kutoka kwetu na miradi ya Wikimedia sasa?" Tulifanya utafiti kuhusu mitindo ya nje ambayo inaathiri kazi yetu, ikijumuisha umakini mkubwa wa taarifa za haraka, ndogondogo; kuongezeka kwa uwepo wa motisha, fedha na vinginevyo, ili kuvutia wachangiaji kwenye baadhi ya majukwaa; vitisho vya kisheria na kisheria, ikiwa ni pamoja na kanuni za jukwaa zinazoweza kutumiwa dhidi yetu na wachangiaji wetu, pamoja na fursa za kuendeleza maslahi ya umma kwa njia chanya; na masuala ya ukweli wa maudhui na athari za Akili Bandia(AI) kwenye mfumo ikolojia wa habari.
  • Usaidizi wa kiteknolojia: Mpango wa mwaka huu pia unasalia kuangazia umuhimu mkuu wa teknolojia, ikizingatiwa jukumu la Shirika kama mtoaji wa jukwaa kwa watu wanaojitolea na wasomaji kote ulimwenguni. Idara ya Bidhaa na Teknolojia ya Shirika ilishirikisha malengo yao mwezi uliopita kabla ya mpango kamili kuwa tayari, ili kuashiria jinsi vipaumbele vyao vya mwaka ujao vinavyoendelea na kukaribisha maoni na maswali. Kwa kiwango cha juu, kazi yetu ya mwaka ujao inalenga kuboresha uzoefu wa watumiaji kwenye miradi ya Wikimedia, kutoa matengenezo yanayoendelea yanayohitajika ili kusaidia tovuti 10 bora za kimataifa na kufanya uwekezaji unaolenga siku zijazo ili kukidhi mabadiliko ya intaneti.
  • Malengo thabiti, kazi ya kurudia-rudia: Malengo manne makuu ya mpango wa mwaka huu pia yanasalia kuwa sawa na ya mwaka jana (Miundombinu, Usawa, Usalama na Uadilifu, na Ufanisi), huku kazi na yanayoweza kufikiwa ndani ya kila lengo yakirudia maendeleo yaliyopatikana katika mwaka huu. Kwa pamoja, malengo hayo manne ni mwongozo wa kuboresha teknolojia inayowezesha miradi ya Wikimedia, kusaidia na kuwezesha jumuiya zetu za kimataifa, kulinda maadili yetu, na kufanya hivyo kwa ubora na kwa ufanisi kwa mwaka huu ujao.
  • Fedha na bajeti: Mpango pia unajumuisha maelezo kuhusu muundo wa kifedha wa Shirika na bajeti yetu. Bajeti ya Shirika inaonyesha mabadiliko yanayoendelea, tunapoona kasi ya ukuaji wa mapato inapungua. Ili kukidhi ukweli huu mpya, Shirika limepunguza ukuaji wake kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kupunguza utumishi na gharama mwaka jana. Tangu 2022, ufadhili kwa mashirika mengine ya harakati umepita kasi ya ukuaji wa Shirika, kitu ambacho kinasalia kuwa muhimu katika mpango wa mwaka huu.

Mwisho, rasimu ya mpango huu inafika wakati wa mazungumzo ya jumuiya kuhusu Mkataba wa Harakati unaopendekezwa, ambao utapigiwa kura na Wanajumuiya hapo mwezi Juni 2024. Kwa kuzingatia kanuni za ukaimishaji na ufanisi, Shirika la Wikimedia Foundation linasalia kujitolea kushirikisha na kuhamisha majukumu ambayo mashirika mengine ya Wikimedia yana vifaa vya kutosha kuweza kumiliki.

Shirika limenufaika kutokana na ushirikiano wa mara kwa mara na wa moja kwa moja na Kamati ya Uandishi wa Mkataba wa Harakati (MCDC), na mazungumzo na washikadau wengi duniani kote ili kufahamisha na kuunda mitazamo yake kuhusu majukumu ya baadaye. Bodi ya Wadhamini na uongozi pia walijadili hali tofauti, ikiwa ni pamoja na MCDC, kutathmini utayari wa Shirika kufanya mabadiliko ya hali ilivyo kuanzia sasa - na bila kutegemea matokeo ya uidhinishaji. Tayari tunatayarisha majukumu haya ili yasimamiwe kwa pamoja na watu wanaojitolea kwani mabadiliko endelevu huchukua muda, na ili kuyafanya vyema, mabadiliko ya kimuundo yatahitaji kuanza kwa mashauriano ya makini kuanzia sasa:

  • Ugawaji shirikishi wa rasilimali: Mnamo 2020, tuliunda Kamati za Fedha za Kanda ili kushauri Shirika kuhusu ugawaji wa rasilimali za kikanda na kufanya maamuzi ya ufadhili kuhusu ruzuku za jumuiya. Mwaka huu, tutaziomba kamati zishirikiane na Shirika kutoa ushauri kuhusu mgao wa kikanda, kutuleta karibu na ugawaji shirikishi wa rasilimali na kuhakikisha usawa zaidi katika kufanya maamuzi ya ruzuku.
  • Baraza la Majaribio la Ushauri wa Bidhaa na Teknolojia: Dhana hii inatokana na Kamati ya Bidhaa na Teknolojia ya Wikimedia Foundation na inafuata mkakati wa harakati wa Baraza la Teknolojia. Mwaka huu, tutajaribu jaribio la kukagua na kushauri kazi ya Shirika la Wikimedia Foundation ya Bidhaa na teknolojia.
  • Mkakati wa Ushirika Ulioboreshwa: Katika mwaka uliopita, Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation ilifanya kazi na Kamati ya Ushirikiano, washirika, na wafanyakazi wa Shirika kuboresha Muundo wa Washirika wa Wikimedia Foundation. Mwaka huu, tutaendeleza mafunzo na kujibu baadhi ya maswali muhimu kutoka kwenye mchakato huo.

Masimulizi ya rasimu ya Mpango wa Mwaka wa muundo mrefu ni maneno marefu 23,000 ili kuhakikisha kuwa yanaweza kutumika kama muhtasari wa kina na pia nyenzo chanzo kwa mawasilisho mengine na muhtasari mfupi. Tunakaribisha maoni na maswali yako katika wiki zijazo kwa namna yoyote unayopendelea: kwenye-wiki kwenye Meta, sehemu za mijadala za miradi ya Wiki husika, na kwa kujiunga na vikao vya mtandaoni vya jumuiya zinazosimamiwa na jumuiya mbalimbali duniani kote.

Asanteni,

Maryana

Maryana Iskander

Mkurugenzi Mtendaji wa Wikimedia Foundation